Edward
Lowassa
Wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisema CCM itazoa
ushindi katika kata zote 25 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao
kampeni zake zinaendelea nchini kote, Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa amesema watashambulia ardhini.
Hatua ya Lowassa inakuja baada ya Mbunge wa Arusha
Mjini (Chadema), Godbless Lema kuzindua kwa mbwembwe juzi kampeni za
udiwani Kata ya Makuyuni, Monduli kwa kutumia helikopta.
“CCM ni jeshi la miguu. Tuko pamoja na wananchi na ndiyo maana tunafungua matawi kwa kishindo,” alisema Lowassa jana.
Lowassa aliyekuwa pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu
Mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine walimrudisha CCM, Mkuu wa Wazee wa
Kimasai, Samuel Soinge aliyekuwa Chadema, walipokuwa wakimnadi Goodluck
Lerunya anayewania udiwani katika kata hiyo.
Akizindua kampeni katika Kata ya Mbalamaziwa,
wilayani Mufindi mkoani Iringa, Kinana alisema: “Kutokana na jeshi kubwa
na wafuasi tulionao na imani inayoendelea kuonyeshwa na wananchi
kuiunga mkono CCM, tuna imani dhamira hii itafanikiwa bila shaka yoyote.
Chadema
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Viwanja vya
Soweto Arusha juzi, Lema alisema chama chake kimepata taarifa kuwa
baadhi ya vyama vimejiandaa kufanya fujo ili kuvuruga kampeni za Chadema
inayopigana kurejesha viti vinne vya udiwani katika Kata za Elerai,
Kimandolu, Kaloleni na Themi.
“Kama jeshi la polisi hawatatulinda, tutajilinda
wenyewe kupitia Red Briged. Tunao uwezo wa kujilinda na kuwadhibiti
wenye nia ya kutuhujumu,” alisema Lema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas
alisema jeshi hilo limejipanga kikamilifu kudhibiti vurugu na uvunjaji
wa sheria kipindi chote cha kampeni na kuvitaka vyama vyote kuzingatia
sheria, kanuni na taratibu.
Akimnadi mgombea wa Chadema Kata ya Kaloleni,
Emmanuel Kessy, Lema aliwaomba wapiga kura kuwachagua wagombea wa
Chadema ili kukipa chama hicho uwezo wa kuongoza Halmashauri ya Jiji la
Arusha.
Singida na Arusha
Akimnadi mgombea udiwani wa CUF katika Kata ya Iseke, Tarafa ya Ihanja, Wilaya ya Ikungi, Singida, Abdallah Kinyeje, Mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mkunduge Kinondoni, Dar es Salaam, Tamim Omari Tamim alisema chama chake hakina udini, ukabila, ukanda, ubaguzi, kupandikiza chuki wala harufu ya vurugu zinazosababisha madhara na Watanzania kupoteza maisha.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Akimnadi mgombea udiwani wa CUF katika Kata ya Iseke, Tarafa ya Ihanja, Wilaya ya Ikungi, Singida, Abdallah Kinyeje, Mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mkunduge Kinondoni, Dar es Salaam, Tamim Omari Tamim alisema chama chake hakina udini, ukabila, ukanda, ubaguzi, kupandikiza chuki wala harufu ya vurugu zinazosababisha madhara na Watanzania kupoteza maisha.
CUF pia kimetamba kuibuka na ushindi katika
uchaguzi mdogo katika kata tatu za Arusha Mjini, kati ya nne kutokana na
kuwa na wagombea wanaokubalika. Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius
Mtatiro alisema: “Hapa Kaloleni hakuna ambaye hamfahamu, Abbas
Mkindi... Elerai kuna John Bayo na Themi yupo Petro Ndalivoi.”
Mwananchi
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment