Kukosekana kwa fedha katika kitengo cha ukaguzi katika idara ya elimu kumetajwa kuwa changamoto kubwa ya kushuka kwa elimu hapa nchini katika miaka ya hivi karibuni.

Kaimu katibu mkuu wa Chama cha waalimu Tanzania CWT Hezekia Oluoch  amesema serikali iboreshe idara ya ukaguzi kwa kutenga bajeti ya kutosha kwa wakaguzi kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Katibu huyo amesema kutokaguliwa kwa shule ni sababu mojawapo ya kushuka kwa elimu hapa nchini, hivyo ameishauri serikali kuwekeza zaidi katika kitengo hicho.

Bwana Oluoch amesema serikali imewekeza kiasi cha asilimia moja nukta nne ya pato la taifa  kulinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo Kenya inatumia asilimia  7.7 Uganda asilimia 4.8, Rwanda asilimia 5.8 na Burundi asilimia 3.2.

Kwa upande wa madai ya walimu katibu huyo amesema itakuwa vigumu kwa walimu kufundisha kwa morali ya juu wakati wana madai mbalimbali ambayo hayajafanyiwa kazi na serikali kwa kipindi kirefu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top