Waziri wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe
Miezi mitano baada ya vigogo 16 wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) kusimamishwa kazi na Waziri wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa
mali za mamlaka hiyo jana imetangaza nafasi za kazi 10, zikiwemo
zilizokuwa zikishikiliwa na vigogo hao.
Katika tangazo lililosainiwa na Mwenyekiti wa bodi
hiyo, lilieleza kuwa watu wanaohitajika ni wale wenye uwezo wa
kitaaluma, kujituma, kujitolewa na waadilifu katika kazi. Desemba mwaka
jana, Dk Mwakyembe alitangaza uamuzi huo ulioafikiwa pia na Bodi ya TPA,
baada ya kupitia ripoti ya kamati iliyoundwa ili kuchunguza tuhuma
hizo.
Hali kadhalika, kuipitia ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Baadaye waziri huyo alitangaza alimwachisha rasmi
kazi aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Emprahim Mgawe na Naibu
wake, Hamad Koshuma.
Wengine ni Naibu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu),
Julius Mfuko, Mkuu wa Kitengo cha Mafuta Kapteni, Massaro Tumaini na
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ngamilo.
Nafasi zilizotangazwa katika tangazo hilo ni ya, Mkurugenzi Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kitengo cha Miundombinu, na Kaimu Mkurugenzi Huduma.
Nafasi zilizotangazwa katika tangazo hilo ni ya, Mkurugenzi Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kitengo cha Miundombinu, na Kaimu Mkurugenzi Huduma.
Nyingine ni Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, Mkurugenzi wa Sheria, Meneja
Mawasiliano, Meneja wa kituo cha Mafuta Bandari ya Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (Tehama).
Waliokuwa wamesimamishwa tangu Desemba mwaka jana
ni Mkurugenzi wa Uhandisi, Bakari Kilo, Mkurugenzi wa Mipango, Florence
Nkya, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Ayoub
Kamti.
Wengine ni Mkurugenzi wa Mfumo wa Menejementi, Dk
Maimuna Mrisho, Meneja wa Uhandisi, Raymond Swai, Meneja Ununuzi na
Ugavi, Bahebe Machibya na Meneja Ununuzi, Theophil Kimaro.
Wengine ni Ofisa Mhandisi Mkuu, Mary Mhayaya,
Meneja wa Tehama, Macelina Mhando, Fotunatus Sandaria wa kitengo cha
Ulinzi, Fadhil Ngorongoro wa Kitengo cha Majini, Mohamed Abdallah
(dereva), Owen Rwebangila na Kilimba wa Idara ya Ulinzi.
katika maelezo yake Dk Mwakyembe alisema baada ya
kamati ya kuchunguza tuhuma za bandari kukamilisha kazi yake, bodi yake
iliipitia ripoti hiyo na kubaini mambo mbalimbali.
Alisema idadi ya vigogo waliosimamishwa kazi hadi wakati huo ilikuwa 23 na kwamba zoezi la kuwasimamisha watumishi wengine litaendelea.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Alisema idadi ya vigogo waliosimamishwa kazi hadi wakati huo ilikuwa 23 na kwamba zoezi la kuwasimamisha watumishi wengine litaendelea.
Mwananchi

0 comments:
Post a Comment