Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa
katika mlipuko uliotokea kwenye kiwanda cha mbolea kilichoko Kaskazini
Magharibi mwa eneo la Waco, jimbo la Texas. Watu wengi wamekwama ndani ya
majengo yanayoendelea kuteketea kufuatia mulipuko huo.
Meya wa Mji kulitokea mulipuko huo, Tummy Muska
ameelezea kutokea moto mkubwa uliolipuka sawa na bomu. Mulipuko huo
umeharibu majengo ya kiwanda hicho, makaazi ya karibu kikiwemo kituo
kimoja cha afya.
Wazima moto, magari ya kubebea wagonjwa na helikopta sita zimetolewa kushughulikia majeruhi na kutuliza hali ya sasa.
Majengo kadhaa yameendelea kuteketea karibu na
kiwanda hicho cha mbolea.Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema
zinasea kuna watu waliopoteza maisha.
Dean Wilson wa idara ya usalama ya Texas amesema nyumba 75 karibu na jengo hilo ziliharibiwa kabisa.
Amesema kufikia sasa hawezi kuthibitisha vifo
vyovyote. Watu 38 wameripotiwa kua katika hali mahututi. Makundi ya
waokoaji yameanza kufika nyumba moja hadi nyingine kuwaokoa majeruhi na kutoa
huduma ya kwanza.
Kituo cha Dharura kimewekwa kwenye uwanja wa
mpira ulioko karibu. Gavana wa Texas amesema afisi yake imetoa raslimali
zake kusaidia katika juhudi za wokozi.
0 comments:
Post a Comment