MAN CITY WAOTA UBINGWA  EPL KUIVAA SPURS

 Kocha wa timu ya  Manchester City, Roberto Mancin
Sergio Kun Aguero
Kocha msaidizi wa klabu ya Manchester City ya England Brian Kidd amesema bado kocha mkuu Roberto Mancini anaamini timu yake itatetea ubingwa ligi kuu nchini England.

Kidd anasema Mancini anajua matokeo yaliyo kinyume na ushindi dhidi ya Tottenham siku ya jumapili ni sawa na kuwakabidhi ubingwa mapema  vinara Manchester  United endapo watashinda dhidi ya Aston Villa siku ya Jumatatu.
Man City watakuwa wakiangalia maendeleo ya washambuliaji wao Sergio Kun Aguero na David Silva kujua namna ya kuwatumia wakitokea katika majeraha.
 Jermaine Defoe
Tottenham itamkosa mshambuliaji wake tegemeo Jermaine Defoe ambaye ni majeruhi huku Aaron Lennon akijikongoja kutoka katika hali hiyo pia Gareth Bale atarejea dimbani kwa mara ya kwanza baada ya kutoka kuwa majeruhi.
Manchester United imecheza mechi 33 ambapo inaongoza ikiwa na pointi 81 ikifuatiwa na mabingwa watetezi Man City wenye pointi 68 lakini wamecheza mechi 32.

Mchuano Mkali zaidi
Timu hizo zinachuana vikali kuwania ubingwa unaoshikiliwa timu hizo hasimu zinazotoka jiji moja la Manchester ambapo ubingwa lazima utue jijini humo lakini ni timu gani itauchukua ni utakaotoa jibu kwa mechi zilizosalia.
Katika kinyang’anyiro cha kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya kumebaki nafasi tatu kwa Chelsea,Arsenal,Tottenham Hotspurs na Everton.Timu nne tu zinatakiwa zitakazoshindwa basi zitalazimika kupigania nafasi ya kushiriki Europa League maarufu kwa hapa nyumbani kama UEFA NDOGO

MOURINHO KUAMUA HATIMA MSIMU HUU
Kocha wa klabu ya Real Madrid, Jose Morinho.  

Kocha Jose Morinho wa klabu ya Real Madrid ya Hispania kuamua hatima yake mwishoni mwa msimu huu.

Baada ya tetesi kuzagaa kocha huyo Mreno amesema cha muhimu kuhakikisha anaifikisha timu yake kwenye mafanikio kisha ataangalia mustakabali wake na uongozi wa klabu hiyo.

Kocha Mourinho ameiwezesha timu ya Real Madrid ambayo ni bingwa wa mara tisa wa UEFA champions league kutinga nusu fainali ambapo itakwaana na Borussia Dortmund ya Ujerumani huku Mahasimu wao wakuu Barcelona wakipambana na mabingwa wa mara nne wa ligi hiyo maarufu ulimwenguni,Bayern Munich pia ya Ujerumani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top