Picha kwa hisani ya mtandao
Barua hii nimeikuta katika mtandao wa kijamii wa facebook nikaona, baada ya kupata ridhaa ya mwenye habari, sio vibaya na wewe ukaisoma.
BARUA YA MWALIMU Tanzania Nchi Yetu Sote KWA RAIS JAKAYA KIKWETE.
Habari yako mheshimiwa Rais?
Kwanza kabisa heshima yako, shikamoo na Pole sana na kazi za
kulitumikia Taifa letu.
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi Matakapola,
iliyopo Ilala hapa Dar. Haina haja ya utambulisho sana, naomba niende
kwenye dhumuni la hii barua.(Ila ombi, naomba hii barua uisome wewe
mwenyewe Rais, kama kuna servant anakusomeaga, aishie hapa. Aiweke store
siku ukiwa na muda wa ziada wewe ndio uisome taratibu.
Tafadhali sana.
Ijumaa iliyopita mshahara wangu uliingia kwenye account yangu. Asante
sana ingawa ni jasho langu. Basi yafuatayo ni matumizi yangu tokea
Ijumaa hadi leo:
1. Kodi ya chumba (miezi 3)- Tsh 60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya umeme Tsh.5,000
2. Chakula cha akiba kwa huu mwezi (Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage 5kg, Mafuta 2Lts)-Tsh 42,000.
3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vitu vidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni kama majani ya chai, chumvi, mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,000
4. Mwalimu usafi, imebidi nipitie mitumbani (huku ni sehemu unakoweza pata kitu cha bei kubwa kwa bei nafuu) nipate nguo za kubadilisha, maana hizi wanafunzi wamenizoea nazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000 na nikazipeleka kwa fundi kuzirekebisha (Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani ni kawaida kuwa oversize, ombea isiwe undersize, na ukishanunua hakuna
guarantee wala kurudisha) hapa nikatumia tena Tsh 5,000. Pia nikaenda
duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5,000), Mafuta ya BabyCare
(Tsh.1000).
5. Wazazi wangu wameteseka sana kunisomesha, hivyo
fadhila muhimu kuwarudishia kwa hiki hiki kidogo nipatacho. Nikawa
M-Pesa Tsh.40,000 ili watumie kubadilisha mboga Juma pili na nusu
iwasaidie kumalizia ada ya mdogo wangu Riziki, yupo ile shule uliyokuja
izindua mwaka 2011/May/13 kijijini kwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi,
sidhani kama unakumbuka, maana ulituahidi visima, barabara, madawati
shuleni na kujenga bweni la wasichana, ila hadi leo umetuachia manyoya.
Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati la drafti
drafti jeupe. Na ulikuja na mama, yeye alivaa full vitenge vya chama!
umeKumbuka?)
6. Kuna hela ya nauli kwenda na kurudi kila siku
shuleni (Tsh.600 per day), vitafunwa asubuhi kila siku (Tsh.200 per
day), na vitu visivyo nunulika kwa wingi, maana vitaharibika kama
vitunguu, sabuni, nyanya, nazi, karoti, nk nakadiria Tsh.10,000 kwa
mwezi.
7. Mheshimiwa kuna vitu havizuiliki kama vocha, nyama
wakija wageni, kwenda hospitali, bado kutoka out mara moja moja (Yaani
kama wewe unavoendaga Sydney kula mbuzi, na sisi tunaendaga kwa mama Lucy
sinza, kula vifaranga).
8. Kuna Hiyo pesa tunaiita hela ya emergence kama michago ya mtaani, sadaka, misiba, kiatu/nguo kwa fundi...etc. Mheshimiwa kama ulisoma vizuri
hesabu kama mimi, roughly hapo ni jumla kama Tsh. 210,000 nikiongeza na
pesa ya hitaji no.7&8 jumla kama Tsh.250,000.
Mheshimiwa kutaja
mshahara wangu hapa si vizuri, lakini, kwakuwa mama hapo nyumbani
ameshawahi kuwa mwalimu naomba nikusumbue, hebu muulize walimu grade A,
tunaoanza kazi tunalipwaje?
Kumbuka hapa bado niko peke yangu
(Single Boy), sina hata mpenzi. Hivi nina ndoto za kuoa kweli ukitizama
iko kipato? Nikiwa na mtoto je? Akianza kusoma je? Nawaza sijui nikakope
NMB au FINCA au VICOBA sijui Bay Port au SACCoS? Yaani sijielewi.
Sikushawishi uniongeze mshahara, ninachoomba tu, fananisha kazi yangu na
hiyo wanayofanya wabunge "wako" niliowachagua, au hata kazi
unayofanya wewe.
Ndiyo. Wewe Mheshimiwa.
Kuna watu wananishauri nianzishe
tuition, lakini mimi ni mzalendo wa pili baada ya Nyerere, itakuwaje
watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this is not fair (Sijui kama umeshawahi waza hili Mh.)
Wengine wamesema nianzishe biashara. Sijui
hata pa kupata mtaji, pili sio vizuri maana nitaelekeza nguvu nyingi
kwenye biashara kuliko kazi ya kuelimisha hili Taifa, narudia mimi ni
Mzalendo.
Hawa waliosema niache kazi wapotezee (achana nao).
Ok Mh, naomba nisiongee sana maana una kazi, safari na mambo mengi sana. Nisikuchoshe.
Natumaini ombi langu (Kama umesahau la kuweka hapo matumizi yako ya mshahara) litasikilizwa na kufanyiwa kazi.
Wako katika kujenga, kuelimisha na kuandaa Taifa lijalo,
Mwl. Tanzania Nchi Yetu Sote.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment