NINAVYOMFAHAMU ZITTO ZUBER KABWE - KILIO CHA USALITI (Sehemu ya Tatu).

Nianze na Nukuu ya Kauli ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Chama Makini (CCM) Ndugu Nape Moses Nnauye, Kama ifuatavyo:-
“..UKIWA MNAFIKI UJANANI, UZEENI UTAKUWA MCHAWI...”

Ninayo nyongeza ya maneno yangu binafsi katika nukuu hiyo, niseme kuwa “Tayari wapo watu wameshakuwa na kukithiri katika Uchawi UJANANI, ni shaka yangu ninapojiuliza UZEENI watakuwa “NANI”.

Jina Langu ni MTELA ALLAM MWAMPAMBA mwanachama mchanga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ninayesoma na kujifunza Ilani, Sera, Miongozo, Kanuni na Taratibu za Chama Changu, ninajifunza katika maandiko ya Chama na najifunza kwa Viongozi wangu kutoka katika kauli zao, maelekezo yao na utashi wao katika Utendaji wao makini unaokisaidia Chama katika kukabiliana na Changamoto mbalimbali kinazokumbana nazo. Najifunza misingi ya kuimarisha na Kukijenga Chama Changu hiki kwa kujitoa kwa dhati ya Moyo wangu na Michango ya Fikra zangu huru.

KABLA ya kuwa mwanachama wa CCM, niliwahi kuwa mwanachama na kiongozi ndani ya Chadema, nikishirikiana kwa karibu zaidi katika Ujenzi wa Chama hiko katika hatua mbalimbali kama nilivyowahi kubainisha katika baadhi ya maandiko yangu.

Kwa anayenifahamu na kuifahamu Chadema na Viongozi wake atakubaliana na ukweli kuwa MIMI, MTELA MWAMPAMBA nilikuwa karibu zaidi na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe.

Masaa machache yaliyopita katika Forum maarufu ya mitandao ya kijamii hapa nchini, Jamiiforums maarufu kama JF, Mhe. Zitto kwa ID yake ambayo ni verified ameandika Thread yenye kichwa cha habari: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/424280-siri-ya-kuuwawa-zitto-uwongo.html
ambapo katika taarifa hiyo ameigawanya sehemu nne:-
i) Ameanza na Ukanusho katika sehemu ya kwanza, akikana kumtambua BEN SAANANE.

ii) Sehemu ya pili ameelezea IMANI yake kubwa kwa DR SLAA, na kudai kuwa SLAA hana sababu ya kumdhuru yeye.

iii) SEHEMU YA TATU akatoa USHAURI na ANGALIZO kwa wale WALIOHAMA chama hiko ( akiwanasibisha na yanayoendelea Chadema Hivi sasa) kuacha kujihusisha ama kukiongelea Chama hiko.

iv) Sehemu ya nne ametoa ushauri kwa Viongozi wenzake wa Chadema kuwa na mshikamano ndani ya Chama hiko.

Nikiwa ni Mwanachama wa CCM, nimeapa kwa Imani ya Chama Changu kuwa NITASEMA KWELI DAIMA NA FITINA KWANGU MWIKO. Kiapo hiki ni ndani ya Chama Changu, Serikali yangu na mbele ya Jamii yangu.

Kwa kuwa LENGO langu si KUFITINISHA wala KUJIHUSISHA NA CHAMA CHAKE, Nitabainisha (kwa Ufupi) namna ninavyomfahamu ZITTO ZUBER KABWE, tena ikibidi nitabainisha kinagaubaga na wazi wazi (kama italazimu kufanya Hivyo) kiasi Umma ubaini ni nani ZITTO ZUBER KABWE ndani ya Chama: mjenzi, nguzo, mhimili ama mhujumu Chama. Nafanya hivyo kwa lengo la kutetea maslahi ya Kitaifa, maana watu hawa wanabeba nembo na sura ya Utaifa, na ni ubaya ulioje watu wasio na DHATI ya kiutawala kuaminiwa katika Utawala.

Na kwa bahati mbaya katika taarifa hiyo nimetajwa tena kwa jina langu kamili, hivyo jukumu la kunyoosha maelezo ya ZITTO ni la msingi na lenye msukumo Binafsi (Si chama Changu kwa namna yeyote)

Ni kwa msukumo huo ninajikuta ninao wajibu wa kuwabainishia UMMA juu ya mambo hayo manne ambayo ZITTO ameyasema.(Kwa maana sitaeleza lini na wapi nimekutana na ZITTO.,sitaeleza tunafahamiana kiasi gani na tuliwahi kupanga lipi na wapi, sitasema tulifanikiwa mangapi na kushindwa mangapi, sitaeleza “sura halisi” ya ZITTO ninayoifahamu mimi kuliko mtu yeyote mwingine katika Chadema (ILA NASISITIZA KUWA NITAFANYA HIVYO TU PALE ITAKAPOBIDI)

Kwanza, nimeipitia kwa Umakini Mkubwa Taarifa hiyo ya ZITTO na kushuhudia UNAFIKI MKUBWA, UPOTOSHAJI NA UONGO ULIOKITHIRI KATIKA BAADHI YA VIPENGELE NA KUJIKOMBA KUSIKO NA HATA CHEMBE YA AIBU WALA SONI kwa mwandishi wa Taarifa ile. 

i) SEHEMU HII YA KWANZA:
Nakubaliana kabisa na Zitto kuwa hakukuwa na kikao ambacho kilitukutanisha Sisi Wanne pamoja, pale LUNCH TIME, kama ilivyoandikwa kwenye GAZETI (kwa mujibu wa ZITO) hayo ni ya mwandishi mwenyewe, maana Mimi si chanzo chake. Lakini hiyo haimaanishi kwamba sisi hatukuwa tukikutana na kujadili Mambo juu ya Chama Chetu (Nikiwa Chadema wakati huo) na Maisha kwa Ujumla wake.

Nimesema sitalieleza hili kwa Undani lakini ukweli uko wazi kuwa taarifa ya SUMU ni ya kweli, na tulikutana na ZITTO nyumbani kwa Kaka yake wa kuzaliwa anayeitwa SALUM OSIBISA pale mkabala na ADA ESTATE Kinondoni, baada ya tukio hilo la SUMU na mjadala wetu uliishia kwa maazimio ya kutokwenda polisi ama kwenye vyombo vya dola kwani kufanya hivyo kungekiharibia CHAMA, lakini kwa hofu ya kushitakiwa na kutaka kujilinda (Defensive Mechanism) BEN alimtuma EXAUD MAMUYA kuja na habari Hapa JF kuwa ZITTO anakihujumu Chama, habari ambayo ZITTO aliikanusha kwa maneno Makali, ambayo hata leo yameendelea kunukuliwa katika maandiko na comments mbalimbali kuwa ametokea kigoma na ikitokea kifo chake kimehusiana na mtu basi mtu huyo kwao hakutobaki kitu. 

Zitto anatambua ni barua ngapi alizoziandika kwa kamati kuu ya Chadema kumshitaki BEN SAANANE na kutaka Kamati kuu imtake BEN athibitishe uongo anaousema juu ya Zitto mitandaoni.

ZITTO na viongozi wengine wanajua nini kimesemwa kuhusiana na Sakata letu ndani ya Kamati Kuu iliyopita na Jinsi hoja hiyo ilivyosababisha Kikao hiko kutahamaki pindi mwenyekiti alipoizima, lakini anafahamu kuwa Kikao Cha Kamati Kuu ijayo kitamjadili yeye (ZITTO) na SHIBUDA na BEN ni miongoni mwa watu watakao toa Ushuhuda wa aliyoyatenda ZITTO katika CHADEMA na juu ya anayoyasema yeye BEN katika mitandao ya Kijamii.

Kama pamoja na yote ambayo yaliyopita na yanayoendelea CHADEMA hadi hivi sasa bado yupo anayeamini maneno ya ZITTO kuwa hamfahamu BEN SAANANE na kuwa anaweza kupishana nae njiani bila kumtambua na aendelee kuamini hivyo lakini nasema hiyo ni too much of exaggeration on his expressions. 

ii) SEHEMU YA PILI:
Nimesema kuwa sitaki kuizungumzia Chadema kiundani, and that fact limit some basic arguments ambazo ningeweza kuzitoa, ila wakati mwingine hata machache katika maneno yenye ukweli na uhalisia watu hujifunza kwayo na huwaongezea utambuzi, nitasema hata machache tu, katika mgogoro mkubwa unaokitingisha Chama hicho hivi sasa ni kile kilichoelezwa kwa Ufupi sana katika SEHEMU YA PILI ya post ya ZITTO ambayo ameileza kipropaganda zaidi na Unafiki mkubwa ambao unalenga kujikomba kusiko na Chembe ya haya, aibu wala soni.

Sikuwa nimeamini mapema niliposoma kipengele hiki “Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo.” Kwa maana yote yanayoendelea Chadema yanatokana na Mvutano na Kadhia ya CHUKI na VISASI baina ya Makatibu wawili wa Chama hiko, hata kuondoka kwangu na wengine ni kafara ya jambo hilo. Kuna mambo si sahihi kuyaeleza kiundani na hadharani kwa sababu tuliambizana na kupanga kwa Usiri na Kuaminiana, hatujafikia hatua hiyo ya kuuvunja hata Uaminifu tuliopeana kwa Viapo ila kama tutaendelea na maneno ya namna hii na UZANDIKI, ipo siku tutayasema.

Kwa kuanzia, Leo nitaweka hapa moja ya Nukuu ya meseji za JOSEPHINE MUSHUMBUSI ya tarehe 22-07-2012 (nikiwa bado mwanachadema) kubainisha Gogoro lililopo baina ya ZITTO na SLAA&MBOWE kama ifuatavyo.

“..nimekusoma uko kigoma kukusanya kadi za chadema, eti zito anapingwa kuwa Rais. Mbona mnatumia nguvu nyingi sana na mikakati iliyovunda! Zito akitaka Urais amuombe Mungu aingie kwenye mioyo ya watanzania siyo Uganga wa Kienyeji, hata wewe ukitaka uenyekiti wa Bavicha behave well. Hakuna Uganga wala uchawi utasimama leo na kesho, mungu anaona mioyo yenu. Hila hazina nafasi jamani kama ulivyo mkakati wenu jaribuni CHAUMA otherwise, si mungu nnayemjua. Naandika haya kuwatambulisha tu upuuzi wote mnaopanga naufahamu. Msijione wajanja saaaana. NA ROHO WANGU MT kama mwalimu wangu ataendelea kunifunulia..’’

Meseji hii ilikuja tukiwa Kigoma na ZITO kwenye Uzinduzi wa Leka Dutigite, ninazo zenye maneno makali zaidi na hata kauli za Slaa, lakini hii inatoa highlight kiasi kuwa issue ni URAIS.

iii) SEHEMU YA TATU:
Nikiwa miongoni mwa waliohama Chadema napokea Ushauri wako wa kuacha kuizungumzia CHADEMA, lakini ingependeza pia ikiwa nanyi mtaacha kuwazungumzia wale waliohama na kuacha kuwahusisha na migogoro yenu na kuwapangia mikakati ya kigaidi.

Kimsingi Ushauri wako huu nimeanza kuufanyia kazi kwenye post hii, wa kuacha kuongelea Mengi kuhusu Chadema na Viongozi wake pia.

Lakini naomba nikushauri kutokana na maneno yako uliyoyaandika leo katika kipengele hiki cha tatu kuwa tusitumie jina lako kufanikisha malengo yetu kisiasa, ni maneno yanayoudhi na kutoka katika misingi ya kulindana. Ni wazi kuwa tumehojiwa katika vikao kadhaa ndani ya Chadema na kote hakuna ambako tulitaja jina lako wala kukuhusisha na chochote kuhusu sisi. Usijiachie sana katika mazungumzo yako, wakati mwingine neno huweza kuzaa yale usiyoyatarajia.
Karata yako ya mwisho inayo-determine maisha yako kama mwanachadema iko mikononi mwetu, Please brother, Don’t mess with your last poker chip, u will lose the game.

Kauli yangu Moja ya Ushuhuda inamaliza Uhai wako ndani ya Chadema., I know you’re smart brother, don’t get crossed., straighten your words..!

Kuwa makini, AND THIS IS SERIOUS…!

iv) SEHEMU YA NNE.
Katika kipengele hiki, nipongeze kwa dhati ushauri huu wa kuwataka viongozi wa Chadema kuacha Fitna, Majungu, Uongo na Uzandiki. Ningependa kuona kuwa kunakuwa na Upinzani Imara hapa nchini ili Chama Changu Cha CCM kiimarike zaidi na kikumbushwe kinapojisahau,lakini si upinzani wa kupinga kila jambo, si upinzani wa mkumbo na uongozi wa ki-imla, si upinzani wa kutohoji na kutoruhusu mawazo na mitizamo huru,si upinzani wa kuchochea vurugu, vitendo vya uvunjifu wa amani na kudhuru watu, si upinzani wa kutukana Viongozi wa Chama Tawala na Serikali, Si Upinzani wa kutamani KUONA NCHI HAITAWALIKI…! 

Tunataka upinzani makini unaosimamiwa na watu walio makini na kwa mtazamo wangu (ambao ninao tangu awali na haujabadilika) Wewe ZITTO unao uwezo, maadili na nidhamu ya kuweza kusimamia Upinzani huo. (nayasema haya kwa kuwa nawajua viongozi Wa CHADEMA, Makao makuu na jumuiya zake)

Mwisho kabisa katika signature yako ya JF umetumia nukuu ya Mwalimu Nyerere kwenye kitabu chake cha TUJISAHIHISHE cha mwaka 1962 mwaka mmoja baada ya Uhuru, kuwa UKWELI haupendi kupuuzwa puuzwa, soma tena kitabu hicho upate hazina ya mawazo ya kiutawala na uondokane na UNAFSI kwa tafsir ya Mwalimu Nyerere ya neno hilo katika kitabu hicho.
VIA: FB
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comments:

Anonymous said... March 29, 2013 at 11:56 AM

Chumvi ikiharibika itatiwa nini hata ifae tena? Hutupa njiani na kukanyagwa na wapita njia.

Ndugu yangu Mtela acha kujitia kiwi ya macho na kujifanya huoni wala huujui ukweli kuwa kwa kipindi hiki cha maisha magumu yenye dhiki iliyotukuka iliyosababishwa na chama unachokiita wewe "makini" (ccm) ni sawa na kujisiriba tope halafu ukajinadi kuwa umependeza ili hali watu wanaokutazama wanakuona kituko

Labda ungeanza kwa kututoa ujinga kuhusu huo umakini unaousema wewe ndani ya ccm ni upi? Je ni ule wa kuhamishia rasilimali za nchi ughaibuni? Je ni viongozi wa juu wa ccm (chama tawala) kujilimbikizia mali na kuzitumia kipindi cha uchaguzi?

Je ni kukumbatia rushwa na kuishabikia hadharani kitu ambacho kilipingwa sana kipindi cha Nyerere? Au ni umakini wa kusaini mikataba kandamizi na ya kinyonyaji dhidi ya wazawa? Je ni umakini wa kuhakikisha wanyonge walio wengi wanaendelea kuwa fukara ili wawe mtaji wa maccm kipindi cha kampeni kwa kupewa Tshts,kofia,kanga na pilau?

Ninapata maswali mengi sana nikikutazama na kusoma makala zako na hasa najiuliza hivi kati ya anayefungamana na wezi,majambazi na wadhulumaji na yule anayetetea maslahi ya umma ni yupi msaliti na mchawi mkubwa?

 
Top