Maseneta wawili wa Marekani John
McCain na Lindsey Graham wamewasili mjiniCairo, wakati jitihada za
kidiploamsia zikishika kasi kuutatua mzozo wa kisiasa nchini Misri
uliozuka baada ya kupinduliwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed
Morsi.
Wasiwasi unazidi kutanda baada ya serikali mpya
inayoungwa mkono na jeshi kutangaza mpango mpya wa kuyasitisha
maandamano, ambako wafuasi wa Morsi wanataka arudishwe madarakani.
Katika siku za hivi karibuni
kumekuwa na wageni mashuhuri wa kiimataifa wanaozuru Misri, wanaotarajia
kusaidia kusimamia kupatikana suluhu ya amani katika hali ya
suitofahamu iliopo kati ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa na serikali
inayoungwa mkono na jeshi.
Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zaidi zimetolewa kuhusu hatua zilizopigwa.
Kwa wakati mmoja kulikuwa na ripoti kwamba
baraza jipya la mawaziri lilikuwa tayari kuwaachia viongozi wa vuguvugu
la Muslim Brotherhood kutoka gerezani na kuwapatia nyadhifa za mawaziri
iwapo watasitisha maandamano mjini Cairo.
Hata hivyo mshauri wa rais amekana tuhuma hizo
na wafuasi wa Morsi wamesisitiza hawatokubali chochote isipokuwa
kurudishwa Morsi madarakani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment