Mwanafalsafa mmoja huamini kuwa watu huzaliwa lakini huishia kufa jambo linalomfanya ajiulize ni kwa nini watu huzaliwa kama kuna kufa?

Matokeo yake huamini kuwa watu huzaliwa, hufanya vurugu saaaaaaana kisha huishia kufa na kufanya maisha yaonekane kama kitu tata. 

Katika kifo twapaswa kujiuliza kama inawezekana tajiri kuwa na mbingu tofauti na maskini baada ya kifo. 

Bila shaka kifo hakina matabaka, tunachokishuhudia ni tofauti katika mchakato wa kuishi, mazishi na ibada.

Mwisho wa yote hubaki kuwa HATUNAYE TENA, kauli inayotumika kwa wote, tajiri au maskini.

Jiulize swali la fujo zako duniani zinapinga au zinachagiza uwepo wa matabaka duniani? TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top