Matokeo
yakidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri)
na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la
sifuri ni mwaka wa tatu sasa mfululizo. Matokeo yakitoka tunasema weeee
mpaka povu linatutoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna hatua yeyote.
Lazima Uwajibikaji utokee.
kwanza
Waziri lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna. Najua
kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa
sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya
mabadiliko. Uwajibikaji ni njia mojawapo inayoleta nidhamu na 'urgency'
katika utendaji kazi.
Tumwambie
Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi
mwakani na yeye atatoka. Najua wa mwakani ndio wapo kidato cha nne sasa
na wana msingi mbaya tayari lakini sio jukumu letu kujipa majibu bali ni
jukumu letu kuiambia Serikali hapana. ...Tuwape Masharti. Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani itakuja nk.
Hawa watoto wanakwenda wapi? Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo
vya ufundi kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti
Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji Tshs 720 bilioni
katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila
Wilaya. Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu ni
Hifadhi ya Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwneye jamii na
ni hatari sana kwa uhai wa Taifa.
Tunaweza kujidai kujenga
madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na
kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya
yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa
mbaya zaidi unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Kawambwa na
wenzake watoke. Watoke SASA!!
0 comments:
Post a Comment