MATUKIO KATIKA PICHA

Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Angetile Osia (kushoto),Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen na Leodgar Tenga wakifuatilia kwa makini sherehe za makabidhiano ya basi maalum la Taifa Stars lililotolewa na kampuni ya bia ya TBL ambao huidhamini kupitia bia ya  Kilimanjaro.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya TBL Robin  na baadhi ya watendaji wa kampuni

Baadhi ya wasanii wa kundi la Wanne Star wakitumbuiza wakati ya hafla hiyo.

Hili ndilo basi la timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambalo limetolewa na kampuni ya TBL ambao ni wadhamini wa timu hiyo. Baadhi ya sifa za basi hilo aina ya YOUTONG ni pamoja na kuwa na TV mbili kubwa,Friji mbili sehemu ya kuwekea vifaa vya michezo,music system yenye spika nane na tanki la kuweka mafuta lita 800,Kiyoyozi na viti 50 kwa ajili ya abiria (wachezaji).

Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah kulia akifuatiwa na Kocha Kim Poulsen,Rais wa TFF Leodgar Tenga, mkurugenzi mkuu wa TBL Robin Goetzche na watendaji wengine wa TBL wakishikilia mfano wa ufunguo wa basi la Taifa Stars kama ishara ya makabidhiano rasmi ya basi hilo tayari kwa kutumika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top