Waziri Benard Membe
MKUTANO wa uhusiano baina ya Tanzania na Oman umemalizika huku viongozi wa nchi mbili hizo wakiamini kuwa uhusiano huo utaimarisha Nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard Membe amesema masuala ambayo wameamua kushirikiana ni biashara na viwanda ,kilimo,ufugaji madini, mafuta na gesi,uwekezaji miundo mbinu kama bandari yamekubaliwa na viongozi wa nchi mbili.

Waziri Membe amesema kilichobakia ni kwa wataalam wa nchi hizo mbili kukutana mara kwa mara ili kuimarisha Nyanja hizo muhimu katika kukuza na kuinua uchumi wa wananchi husika.

Waziri huyo amesema serikali itajenga mazingira ya kuwezesha kampuni na watu binafsi kufanya biashara na kuwekeza katika biashara na sekta nyingine na kuchochea maendeleo.

Tayari serikali ya Oman imeonesha ari hiyo kwa kuomba nafasi ya ofisi kabla ya kujenga jengo la kitega uchumi la Oman kwa ajili ya kufanya shughuli zake hapa nchini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top