Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2012 yametangazwa ambapo kiwango cha ufaulu kimeshuka ikilinganishwa na mwaka jana 2011.Watahiniwa wapatao laki mbili elfu arobaini na mia tisa na tatu (240,903) wamepata daraja sifuri huku watahiniwa laki moja na elfu tatu na mia tatu na shirini na saba (103, 327) wakiambulia daraja la nne.
Imeelezwa zaidi kuwa watahiniwa elfu kumi na tano na mia nne na ishirini na sita (15, 426) wamepata daraja la tatu , watahiniwa elfu sita na mia nne hamsini na tatu ( 6, 453) wamepata daraja la pili huku watahiniwa elfu moja na mia sita na arobaini na moja (1,641) wakipata daraja la kwanza.
Imeelezwa kuwa sababu za kushuka kwa matokeo haya ni uhaba wa waalimu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Kumi Bora Kitaifa
- St Francis ya Mbeya.
- Marian Boys ya Pwani.
- Feza Boys DSM.
- Marian Girls Pwani
- Rosmini ya Tanga.
- Canossa DSM.
- Jude Moshono ya Arusha.
- St Mary Mazinde Juu Tanga.
- Anwarite Girls ya Kilimanjaro.
- Kifungilo ya Tanga.
Aidha imeelezwa kuwa matokeo ya wanafunzi ishirini na nane elfu na mia tano na themanini na mbili (28, 582) yamezuiliwa kwa kutolipa ada ya mtihani TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment