Zaidi ya maduka 16 yameungua moto eneo la kituo cha mabasi cha Mwenge jijini Dar es Salaam kwa kile kinachodaiwa hitilafu ya umeme kusababisha moto mkubwa na kuunguza mali zilizokuwemo na miundo mbinu ya majengo hayo kuharibiwa vibaya.
Kamanda wa
polisi wa kikosi cha Zimamoto kanda maalum Dar es Salaam BAKARI MRISHO amesema
hakuna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa
kutokana ajali ya Moto uliozuka ghafla majira ya saa nne asubuhi.
Kwa mujibu
wa kamanda wa kikosi cha zimamoto kanda maalum Dar es Salaam,amesema chanzo cha moto huo kilitokana na shoti
wakati fundi mmoja alipokuwa akichomelea duka la jirani na eneo hilo.
Kamanda Mrisho
amesema kikosi cha zimamoto kilifika mapema na kuzima moto huo kwa wakati na
kufanikiwa kuuzima na kuongeza kuwa kuna umuhimu kwa wananchi kupewa elimu ya kuepuka ajali ya
namna hiyo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ulizuka ghafla na kuwaka kwa kuruka kuanzia duka moja baada ya jingine na kuteketeza mali zilizokuwemo ambazo ni pamoja na vipodozi, mapambo,viatu na mali nyinginezo.
Hata hivyo
baadhi ya mashuhuda na wamiliki wamesema licha ya mali kuokolewa mapema baadhi zimeathiriwa na kuharibiwa na maji yaliyotumika kuzimia moto
husika hivyo kujikuta wanaingia hasara maradufu.
Hakuna tathmini kamili ya hasara iliyotolewa kutokana na uharibifu huo
uliotokana na ajali ya moto. Hakuna kifo chochote kilichoripotiwa kusababishwa na moto huo.
PICH
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
PICH
0 comments:
Post a Comment