MAN CITY YAIKANDAMIZA CHELSEA 2-0
 Wachezaji Wa Man City
 Mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City wameandikisha ushindi mkubwa dhidi ya mabingwa wa ulaya Chelsea na hivyo kufufua matumaini yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka wa pili, licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka wa vinara wa ligi hiyo kwa sasa Manchester
United.

Mechi hiyo iliyokuwa na mashambulizi na kila aina ya vivutio baina ya timu hizo zinazomilikiwa na matajiri wawili tofauti,imemalizika kwa ushindi wa Man City wa mabao mawili kwa bila.
Mabao ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Carlos Tevez yalitosha kuizamisha Chelsea, na kufufua matumaini ya Man City, kutetea taji lao ambalo sasa linaonekana kuwa mikononi mwa majirani zao Manchster United wanaoongoza ligi wakiwa na tofauti ya point 12.

Mapema kipindi cha pili, Chelsea, walipata penat baada ya Demba BA, kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Man City, Joe Hart, lakini penat iliyopigwa na nahodha wa Chelsea, Frank Lampard, ilipanguliwa Joe Hart na kuamsha mashambulizi zaidi ya Manchester City.

Yaya Toure kunako dakika ya 63 alipenyeza shuti la wastani pembeni mwa lango la Chelsea na kuwafanya Manchester City, kuongoza kwa bao moja kabla Chelsea, kufanya juhudi za kutaka kusawazisha lakini wakajikuta wanoangezwa bao la pili maraidadi kabisa lililofungwa na Carlos Tevez ambaye aliingia akitokea benchi,huku likiwa bao lake la kwanza baada ya mechi sita alizocheza bila kuifungia timu yake.

Kwingineko,katika mchezo mwingine wa leo, Newcastle wakiwa nyumbani,walitoka nyuma baada ya kufungwa bao la mapema na kuchomoza na ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Southampton.

Mabao wa Newcastle yamefungwa na Musa Sisoko,Papis Demba Cisse,Yohan Cabaye aliyefungwa kwa mkwaju wa penati huku bao la nne watakatifu au Southampton wakijifunga.

Mabao ya Southampton yalifungwa na Morgan Scheneiderlin dakika tatu tu baada ya mchezo kuanza huku bao la pili likifungwa na Rickie Lambert. Hata hivyo ushindi wa mabao 2 – 0 wa man city  dhidi ya Chelsea umefanya timu hiyo kupunguza pengo kutoka pointi 15 hadi 12 dhidi ya vinara Man United ambao waliibuka na ushindi magoli wa 2 – 0 dhidi ya Queens Park Rangers QPR.

             MAN UNITED YAIKANDAMIZA QPR  2-0

 
Ryan Giggs Akifunga bao

Ligi kuu ya soka nchini England, imechezwa wikiendi iliyopita kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbali mbali. Huko Loftous Road, Manchester United imeebuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya QPR, huku mshambuliaji Ryan Giggs akifunga bao la pili na kufikisha mabao 999 toka aanze kucheza soka la ushindani na kuifanya timu yake ya Manchester United, kuongeza tofauti ya point 15 na mabingwa watetezi Manchester City.

United ilipata bao lake la mapema kupitia kwa Rafael Da Silva ambaye alifunga kwa shuti kali dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinda mlango wa QPR,Julio Cesar kuokoa kiki la Robin Van Persie.

Rafael ambaye mdogo wake,Fabio yupo QPR kwa mkopo,hii leo alionekana kuwa kwenye kiwango kizuri na kuokoa hatari kadhaa langoni mwa United hasa baada ya kuokoa mpira wa kichwa wa Criss Samba ambao ulikuwa uingie nyavuni.

Licha ya Dan Welbeck na Wayne Rooney kuingia wakitokea benchi,hii leo hawakuweza kupata bao katika ushindi huo ambao unawabakisha United kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka nchini England.

Matokeo haya,yanaendelea kuwabakisha QPR kwenye nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi hiyo yenye upinzani mkubwa duniani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top