HILI NDILO LORI WALIMOPANDA VIBARUA HAO WA SHAMBA LA KAPUNGA
 MTOTO ALIYEJERUHIWA AKIHAMISHWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA NA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
 MAJERUHI AKISUBIRI KUPATA MATIBABU

HAWA NI MAJERUHI
KWELI MUNGU NI MKUU HUWALINDA WATOTO WADOGO HAPA MKUU WA MKOA AKIMPA POLE MOJA YA WATOTO WALIOPATA AJALI
MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI
HILI NI ENEO LA TUKIO

HAWA WOTE NI WANAFUNZI WALIOKUWA WANAENDA KUFANYA KIBARUA CHA KULIMA KWA MWEKEZAJI KATIKA SHAMBA HILO LA KAPUNGA

MMOJA KATI YA MAJERUHI
MAJERUHI 22 WAKIPAKIZWA KATIKA ROLI AINA YA FUSO TAYARI KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
MAJERUHI WAKIWA KATIKA GARI AINA YA FUSO TAYARI KUSAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA RUFAA  MBEYA
MAJERUHI WAKISAFIRISHWA KWENDA MBEYA

WATU watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya  huku hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha  Mapogolo kata ya Itamboleo  Wilayani Mbarali Mkoani hapa.

Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo  ambalo ni mali ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha  Kapunga.
  " Lori hilo lenye namba za usajili T398 BSE aina ya Scania Tipa, ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina  Baraka Moreli, lilionekana likiwa katika mwendo kasi na   dereva huyo akiwa na lengo la kutaka kuipita pikipiki  iliyokuwa mbele yake. Huku akishangiliwa na vibarua hao ipite ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa" moja ya majeruhi alisema.  Aliendelea kusema dipo walipofika kwenye kona dereva gari lilimshinda hilo lilimshinda na kupinduka

   Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika  ajali hiyo  ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.

Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa madaktari,  vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda kuokoa maisha ya majeruhi hao.


Kandoro, alisema kuwa  katika ajali hiyo watu watano wamefariki, wanne wa kiume na mmoja ni mwanamke.Watatu wametambuliwa. Aliwataja waliotambuliwa kuwa ni  Samweli Mapugilo Mbena (30) mkazi wa Ilembula, Bon Mfupa (27) mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile (35) mkazi wa Nonde, Mbeya
VIA MBEYA YETU TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top