Mratibu wa sherehe za mwaka mpya kwa Wachina waishio Tanzania,mwalimu AO MAN YU (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya mwaka mpya yatakayofanyika jijini Dar es Salaam mapema mwezi ujao.
Baadhi ya waratibu wa tamasha la mwaka mpya wa Wachina waishio Tanzania wakiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na maadhimisho yatakayofanyika Februari 2 – 3 mwaka huu.
Baadhi ya viongozi wa chama cha wahandisi washauri Tanzania wakiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama cha Wahandisi washauri Tanzania Injinia Menye Manga (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa kimataifa wa wahandisi utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia leo

Raia wa China wanaoishi Tanzania wanataraji kusherehekea mwaka mpya Februari 2-3 mwaka huu kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazoutambulisha utamaduni wa China.
Mratibu wa shughuli hizo mwalimu wa Kiswahili wa Chuo cha Mawasiliano huko CHINA,AO MAN YU amesema kwa miaka mitatu iliyopita wamekuwa wakiadhimisha sherehe hizo hivyo kwa mwaka huu utakuwa wa NNE tangu waanze kufanya hivyo hapa nchini.
Mratibu huyo amechukua fursa hiyo kuwakaribisha watanzania kushiriki katika shughuli hiyo muhimu ambayo itaambatana na michezo ya asili ya China kama vile kungfu,karate Muziki wa asili ya china na burudani nyingine.
 Mwakilishi huyo wa China amesema Watanzania  wamekuwa WABIA wakubwa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo zikiwemo,utamaduni na biashara.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa inaonesha kwamba Februari 2 shughuli za kimichezo zitafanyika katika viwanja vilivyo jirani na hoteli ya Golden Tulip kuanzia saa 10.00 -  12.00 jioni.Siku itakayofuata kutakuwa na tamasha katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 12:00 – 20:00.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top