Kaimu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu ya mashirika ya umma (POAC) Muhammed Amour Chombo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea ripoti ya shirika la utafiti na  maendeleo ya viwanda Tanzania TIRDO, 
Profesa Idrisa Mushoro mwenyekiti wa bodi ya TIRDO wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya shirika hilo mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu ya Mashirika ya Umma (POAC).
Kamati ya bunge ya  hesabu za mashirika ya umma imekataa ripoti ya fedha iliyotolewa na shirika la maendeleo ya viwanda Tanzania TIRDO kwa makosa ya kimahesabu.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Muhammad Chombo amesema dosari iliyojitokeza katika  bajeti ya shirika hilo ni  milioni 60 ambazo hazijulikani ziliko huku zimetumika milioni 155 kati ya milioni 216.
Kaimu Mwenyekiti huyo amesema kukosekana kwa fedha hizo kwenye akaunti na kwenye maelezo ya ripoti ya TIRDO kunaashiria kuwepo kwa ubadhirifu hivyo kuitaka ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali CAG kulichunguza shirika hilo.
Kamati hiyo imetoa onyo kwa kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo Ludovick Manege kutopindisha ukweli wa maelezo ya ripoti vinginevyo itaonekana kuwa yuko nyuma ya madudu yote yanayofanyika katika shirika hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top