Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi, Mh. Dk. Ali Mohamed Shein |
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza serikali yake
itaendelea kusaidia sekta ya habari na mawasiliano visiwani humo ili kuchangia
kikamilifu katika maendeleo
Akizungumza huko Rahaleo, Mjini Unguja, mara baada ya
kufungua mitambo ya Dijitali na jengo la studio ya kurekodia muziki Dk.
Shein amesema juhudi za makusudi
zitaendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuhakikisha sekta hiyo inaimarika na
kurejea katika uwasilia wake.
Amesema kuwa Zanzibar ina historia kubwa katika sekta
hizo na kuutaka uongozi na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar
kubadilika na kutofanya kazi kwa mazoea
Amesema kuwa
juhudi kubwa zinachukuliwa na serikali ikiwa ni pamoja na kutenga fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo
ya digitali
Dk. Shein amesisitiza kuwa wananchi wengi wa Zanzibar
bado hawajaridhika na wamekuwa wakinung'unika juu ya ufanyaji kazi wa
televisheni na redio ndani ya Shirika la Utangazaji ka Zanzibar (ZBC).
Awali Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Ali Mwinyikai, amewataka wananchi visiwani humo kuwa na subira kwani jambo kubwa
lililochelewesha Zanzibar kuingia kwenye Digitali ni kutaka kuingia katika
mfumo huo kwa uhakika zaidi ikiwa ni pamoja na kuwa na vingamuzi vilivyobora
baada ya kufanya utafiti
Ujenzi wa miundombinu ya Dijitali visiwani Zanzibar
unaosimamiwa na kampuni ya Agape umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 8
0 comments:
Post a Comment