Waziri wa Afya Dkt Hussein Mwinyi amemteua Prof. Samwel Victor Manyele kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Taarifa iliyotolewa na wizara na kusainiwa leo na msemaji wa wizara ndugu Nsachris Mwamwaja imesema kuwa Uteuzi huu unaanza tarehe 21.01.2013. Kabla ya uteuzi huu Prof. manyele alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Awali nafasi hiyo ilikuwa wazi baada ya aliyekuwa mkemia mkuu wa serikali Dkt. Ernest Mashimba kufariki dunia  tarehe 19 Septemba, 2010.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top