Leslie Liunda |
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua
ofisa wake Leslie Liunda wa Tanzania kwenda Ethiopia kukagua viwanja na hoteli
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji leseni kwa klabu
zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari
2 mwaka huu) ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 6 mwakani na
baadaye kupeleka ripoti yake CAF.
0 comments:
Post a Comment