Via Mtandao-net
Magari mawili yamepata ajali jana katikati ya mlima Kitonga. Chanzo cha
ajali hiyo ni lori lenye namba T 722 ACJ lililobeba vifaa vya ujenzi
lilishindwa kuupanda mlima huo na kuanza kurudi nyuma. Wakati
linarudi nyuma kulikuwa na gari aina ya Toyota Corolla yenye namba T 138
ART ikitokea Kilombero kwenda Iringa iliyobeba watu wanne ikiendeshwa
na dereva aliyejitambulisha kwa jina moja la Omary. Ikiwa kwenye mwendo
kasi ilimbidi dereva wa gari hilo (Toyota) kutumbukiza gari lake kwenye
bonde kubwa la mlima huo umbali wa kama mita 45 kutoka juu ya barabara ili kuepuka kuumana uso kwa uso na lori.
Hata hivyo, hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.Shuhudia picha za matukio katika ajali hiyo.
Mtu pekee aliyejeruhiwa katika ajali hiyo, alikuwa kwenye TOYOTA |
Huko bondeni ndiko lilikotumbukia gari dogo (TOYOTA) |
Kijana wa kimasai akiwa amebeba spika ya gari lililopata ajali |
Gari lililopata ajali likiwa bondeni |
Gari lililopata ajali likiwa limenasa kwenye miti |
Baadhi ya abiria wakiwa wamepumzika wakisubiri uokoaji ukamilike ili waendelee na safari. |
Lori lililopata ajali na kusababisha ajali ya gari jingine likiwa katikati ya barabara. |
Dereva wa gari lililosaidia kuvuta lori lililopata ajali alidai alipwe pesa ndipo atoe msaada huo, hapo akikabidhi pesa zilizochagwa na baadhi ya abiria ndipo aanze kazi ya uokoaji. |
Haikuwa kazi rahisi kulivuta gari hilo |
Uokoaji wakamilika |
Nondo zikavutwa kwa gari, abiria wakazivuta kwa mikono |
0 comments:
Post a Comment