|
Nyaya za umeme za TANESCO zikiwa zimetelekezwa katika eneo la Nsenga Mbeya Vijijini. Eneo hili liko mpakani na Jiji la Mbeya |
|
Nyaya hizi zimeshika kutu. Huenda ni baada ya kubaki katika eneo hili kwa muda mrefu. |
|
Nyaya za umeme za TANESCO zikiwa kama vile hazina mwenyewe au zimekosa matumizi. | | |
|
|
|
|
Mwanablog akiwa katika pitapita leo tarehe 22.12.2012 majira ya saa tano amefanikiwa kuzikuta nyaya za umeme za TANESCO ambazo inaonekana zimetelekezwa. Inawezekana kwa vile hazifai. Kwa upande mwingine ukiangalia kwa jicho la kawaida zinaonekana kama vile zinafaa au zilikuwa zinafaa kutumika kabla ya kutelekezwa katika eneo huili.
Kubwa zaidi ni kuwa hivi wanamsubiri Rais au waziri atoe mwongozo wa uhamishaji nyaya hizi wakati watendaji wanaohusika wapo? Au, tunahitaji mwekezaji afanye kazi ya kuhamisha mali kama hizi kutoka ziliko hadi katika eneo sahihi? Msomaji unaweza kujiuliza maswali zaidi. Bila shaka wahusika wanaweza kutuambia kwa nini nyaya hizi zipo mahali hapa hadi kushika kutu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment