Wachezaji wa Taifa Stars wakitoka nje ya uwanja kwa mapumziko baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwenye uwanja wa Taifa.
Ngasa Akishangilia na wenzake goli alilofunga
Timu ya Taifa Tanzania imefanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) kwa bao1-0 katika mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kurushwa na Star TV.  

 Wakicheza kwa kujiamini, ilibidi wasubiri hadi dakika arobaini na tano zifike ndipo mchezaji Mrisho Ngasa aliweza kupachika bao la pekee kwa timu hiyo. Ngasa akikimbia kwa kasi aliweza kuizidi beki ya Chipolopolo mbio na kuachia shuti kali lililomwacha Kipa wa Chipolopolo akiruka bila mafanikio yoyote na kuuacha mpira ukijaa wavuni.


Katika kipindi cha kwanza Taifa Stars ilitawala zaidi sehemu ya kati jambo lililowafanya kucheza kwa kujiamini zaidi. Katika kipindi cha pili Zambia walifanya mabadiliko kwa kumtoa nahodha Christopher Katongo. Mabadiliko haya yaliinufaisha Chipolopolo kwa vile katika kipindi hiki waliweza kutawala zaidi sehemu ya kiungo.

Mnamo dakika ya sita Mchezaji wa Chipolopolo alikosa bao baada ya shuti lake kugonga mwamba. Taifa Stars walijibu mashambulizi ambapo Shomari Kapombe aligonga mpira kwa kichwa uliogonga mwamba. katika dakika ya 54 mchezaji wa Chipolopolo James Chamanga alipiga shuti lililotoka nje.Dakika za 74 na 75 zilikuwa ngumu kwa pande zote ambapo Chipolopolo walifanya shambulizi lililojibiwa na Taifa Stars. Mashambulizi yote hayakuzaa matunda.

Katika mchezo huo  mnamo dakika ya 41 golikipa wa Timu ya Taifa Juma Kaseja alioneshwa kadi ya njano kwa kosa la kuchelewesha mpira. Kwa upande wa Zambia mchezaji Felix Katongo alioneshwa kadi ya njano katika dakika ya 78 kwa mchezo mbaya. 

Hadi dakika ya tisini inafika Taifa Stars moja na Timu ya Taifa ya Zambia haikupata kitu.

Picha via shaffidauda.com 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top