Kikosi cha Yanga |
Mabingwa mara mbili mfululizo wa
Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki al maarufu(Kagame Cup )timu ya Young
Africans inatarajia kuondoka alfajiri ya Jumapili kuelekea nchini Uturuki
ambako itaweka kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki mbili.
Akiongea na waandishi wa habari
makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya
Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika
la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27
na viongozi 7.
Timu itaondoka majira ya saa
10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa 5 kasoro
dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa
Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa
itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'
Kizuguto amesema timu itafikia
katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na
itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel
hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Majina ya watakosafiri keshokutwa
alfajri ni:
Walinda
Mlango: Ally
Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul
Walinzi
wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na
Oscar Joshua
Walinzi
wa kati: Mbuyu
Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani
Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo,
Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme
Viungo wa
Pembeni: Saimon
Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said
Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza
Viongozi watakaoambatana na timu
hiyo ni
Kocha
Mkuu: Ernest
Brandts,
Kocha
msaidizi: Fred
Felix Minziro,
Kocha wa
makipa: Razaki Siwa,
Daktari
wa timu: Dr.Suphian
Juma,
Meneja wa
timu: Hafidh
Saleh,
Afisa wa
Habari : Baraka Kizuguto
na
kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya
utendaji wa klabu ya Yanga
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment