Umekuwa mwisho wa mwaka  mzuri kwa timu ya Azam ya vijana walio chini ya miaka 20 na ile ya wakubwa baada ya kutwaa vikombe katika michuano iliyoshiriki na kumalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.


Wakati  Azam ya wakubwa  ikitwaa kombe la Hisani michuano iliyofanyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo timu ya vijana U-20 imetawazwa mabingwa wa michuano ya Uhai inayoshirikisha timu za vijana za klabu za ligi kuu Tanzania bara.



Timu ya Azam iliyokuwa Congo imetwaa ushindi baada ya kuwabwaga wenyeji Dragons kwa penalty 4 – 2  kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa.



Azam iliingia fainali hiyo  baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.

Kikosi cha Azam kilichoshiriki mashindano haya ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.

Katika mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matatu, ukiachilia mbali mawili ya penati.

Picha via Mtandao wa AZAM