AJALI IMETOKEA LEO MAJIRA YA SAA SITA MCHANA KATIKA ENEO LA NZOVWE JIJINI MBEYA KWA KULIHUSISHA LORI LILILOMSHINDA DEREVA BAADA YA BREKI KUSHINDWA KUFANYA KAZI KATIKA MTEREMKO WA SIMIKE. DEREVA WA LORI ALITOA TAHADHARI ZOTE KWA KUPIGA HONI NA KUWASHA TAA ZA HATARI HATA HIVYO,LOLI HILO LILIPOFIKA ENEO LA KITUO CHA DALADALA CHA NJIAPANDA YA ITENDE LILIZIGONGA DALADALA MBILI KWA NYUMA NA KUSABABISHA ABIRIA WALIOKUWA NDANI KUJERUHIWA VIBAYA. MAJERUHI HAO WALIKIMBIZWA HOSPITALINI KWA MATIBABU. HATA HIVYO, LORI HILO LILIWEZA KUSIMAMA UMBALI WA MITA KARIBU MIATATU KUTOKA KATIKA ENEO LA AJALI. DALADALA ZOTE ZILIKUWA ZINATOKA MWANJELWA KUELEKEA TAZARA. PICHA NA MWANABLOG WAKO.
Daladala ikiwa imeharibiwa vibaya.
Sura ya ndani ya daladala iliyopata ajali
Hali ilivyokuwa kwa viti vya nyuma baada ya majeruhi kuondolewa katika daladala hii.
Mashuhuda wa tukio wakiangalia daladala iliyogongwa.
Hali ilivyokuwa kwa daladala hii.
Hiki ni kipindi cha maandalizi ya krismasi. Hii ni sura halisi ya daladala kwa mbele baada ya kugongwa kwa nyuma na lori.
Lori lililogonga Daladala mbili likiwa limesimama eneo la pundamilia Iyunga.
Lori lenye namba za usajili T 721 BYD lililosababisha ajali  likiwa limesimama..

Sura ya mbele ya lori lililogonga daladala.
Watu wakishuhudia daradara iliyogongwa na kusababisha maafa.
Daradara ikiwa imeharibika vibaya.
Daladala ambayo namba yake ya usajili haikuonekana kabisa ikiwa mtaroni baada ya kugongwa kwa nyuma na lori lililomshinda dereva kutokana na tatizo la breki. Kwa pembeni watu wanashuhudia.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top