Wezi wa mifugo weanaoshukiwa kuwa Wafulani wamewaua watu 79 katika kijiji kimoja Kaskazini mwa Nigeria katika jimbo la Zamfara.
Vyombo vya habari nchini Nigeria mnamo Jumapili
vilimtaja Msemaji wa Gavana wa jimbo hilo, Bwana Nuhu Salihu Anka,
akisema kuwa watu hao waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wezi wa mifugo
kutoka jamii ya Fulani, ambao ni wachungaji.
Maafisa wakuu katika Serikali ya jimbo la
Zamfara walihudhuria mazishi ya watu hao 79 katika eneo hilo hiyo jana.
Naye msemaji wa polisi wa Taifa, Lawal Abdullahi alisema kuwa watu 30
waliuawa katika shambulio la Jumamosi wakati wachungaji waliokuwa na
bunduki kutoka jamii ya Fulani walipovamia mkutano wa wajumbe kutoka
Majimbo ya Zamfara, Kaduna, Kebbi na Kastine wakijadiliana changa moto
za usalama katika maeneo yao.
Anka anatajwa kusema kwamba wamekuwa
wakikabiliana na mashambulizi mabaya sana ya magenge ya watu wenye
silaha na wezi wa ngombe lakini shambulio hili la sasa ndiyo baya zaidi.
Kiongozi mmoja wa kijadi amenukuliwa akisema
idadi ya waliokufa ni wengi zaidi. Alisema hadi kufikia Jumapili
walikuwa wamewazika watu 120 kutokana na shambulizi hilo na kuwa idadi
hiyo inatazamiwa kuongezeka zaidi.
BBC
0 comments:
Post a Comment