Mbu
Utafiti wa kisayansi umebaini kuwa mbu jike wanaoambukiza
vijimelea vya ugonjwa wa Malaria
huvutiwa zaidi na harufu ya mwili wa binadamu kuliko wadudu wengine.
Watafiti waliochapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la Plos One,
wanaamini kuwa Mbu wanaobeba viini vinavyosababisha Malaria, huwa na uwezo
mkubwa wa kunusa.
Daktari James Logan, kutoka chuo cha mafunzo ya fya mjini London, anasema
kuwa moja ya mambo ambayo humshangaza ni ambavyo viini vinakuwa na akili
nyingi.
Anasema kuwa viini vinaonekana kuwa na akili nyingi kiasi cha kuwa mbele kwa
fikira kuliko hata wanasayansi.
Katika kufanya utafiti wao, wanasayanyi waliwaambukiza mbu na viini hatari
vya Plasmodium falciparum.
Waliwaweka mbu hao katika mkebe pamoja na soksi iliyokuwa inavunda na
ambayo ilikuwa imevaliwa kwa masaa ishirini. Mbu hao walijazana kwenye soksi
hiyo,Wanasayansi hao walifanya utafiti huo na mbu ambao walikuwa hawana viini
hivyo.
Waligundua kuwa mbu waliokuwa na viini waliweza kuvutiwa zaidi na soski
zilizokuwa na uvundo.
Wanasayansi wanaamini kuwa mbu waliokuwa na viini wanakuwa na uwezo mkubwa
zaidi wa kunusa kwa sababu viini ndivyo vinawawezesha kunusa zaidi.
Kwa Mmbu, binadamu anakuwa rahisi kushambulia kwa sababu ya harufu ya mwili
wake na kisha viini hivyo ninavamia damu yake kuhakikisha kuwa vinaendelea
kuzaana.
Watafiti
hao sasa watafanya utafiti wa miaka mitatu kutaka kujua ni vipi viini vina
uwezo wa kufanya hivyo.
Daktari
Logan , anasema kuwa ikiwa wataweza kujua viini vinavyosababisha Malaria,
itawasaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Kulingana
na takwimu za hivi karibuni, shirika la afya duniani linasema kuwa mnamo mwaka
2012, takriban watu milioni 219 waliugua Malaria huku wengine 660,000
wakiripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo.
Afrika
ndilo bara lenye visa vingi vya watu kuugua Malaria na asilimia tisini ya vifo
vinavyotokana na Malaria hutokea barani humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment