Gideon Mwakanosya, Songea
WATU
watatu wamefariki dunia na wengine 24 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi
waliokuwa wakisafiria kutoka songea kwenda mbeya kumgonga mwendesha
baiskeli na baadaye kupinduka.
Habari
zilizopatikana leo mchana mjini Songea ambazo zimezibitishwa na
kamanda wa polisi mkuo wa Ruvuma Mihayo Msikhela zimesema kuwa tukio
hilo limetokea jana majira ya saa nne na dakika 45 asubuhi katika eneo
la Sanangula nje kidogo na manispaa ya Songea.
Kamanda
Msikhela amefafanua kuwa ajali hiyo imetokea kwenye barabara ya kutoka Songea kwenda Njombe ambako namba za gari za usajili T273 CDD aina ya
Mistubishi Rosa mali ya kampuni ya Super Feo ambalo lilikuwa linatoka Songea kwenda Mbeya.
Ameeleza
zaidi kuwa basi hilo likiwa kwenye mwendo kasi mbele yake kulikuwa na
mwendesha baiskeli ambapo dereva wa gari hiyo aliyejulikana kwa jina la Steven
Mbigi (45) baada ya kumkwepa mwendesha baiskeli aligonga mti na
kupinduka na kusababisha watu wawili kufariki dunia papohapo.
Alisema
kuwa mwendesha baiskeli alijeruhiwa
vibaya hivyo pamoja na majeruhi wengine walikimbizwa katika hospitali ya
mkoa kwa matibabu ambako alifariki dunia akiwa chumba cha wagonjwa mahutihuti
wakati madaktari wakiendelea kumpa matibabu.
Kamanda
Msikhela alisema kuwa maiti za watu hao wawili bado hazijatambuliwa lakini maiti zote 2 zimehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia mahiti kilichopo katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma ya Songea
Amesema kuwa majeruhi wote 24 pia majina yao hayajatambulika na wamelazwa katika hospitali hiyo ambako wanaendelea kupata matibabu.
Msikhela
amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi
hilo Mbigi mkazi wa mtaa wa Ruvuma Manispaa ya Songea ambaye inadaiwa
amekimbia mara tu baada ya ajali hiyo na polisi inaendelea kumsaka.
Kwa
upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Dr. Benedictor Ngaiza
amethibitisha kupokea majeruhi 25 ambao mmoja kati ya majeruhi hao
aliyejulikana kwa jina la Aron Edward ambaye alikuwa amelazwa katika
chuma cha uangalizi maalum(ICU) alifariki dunia wakati akiendelea kupata
matibabu
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment