MTU MMOJA AMBAYE HAKUWEZA
KUTAMBULIKA JINA WALA MAKAZI YAKE AMEKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA
USONI.
TUKIO HILO LIMETOKEA
MNAMO TAREHE 11.09.2014 MAJIRA YA SAA 07:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA ILOLO, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI. KATIKA ENEO LA
TUKIO, KUMEKUTWA GODORO MOJA JIPYA, MASHUKA MAWILI NA SKETI MOJA RANGI
NYEUSI.
MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA
MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI NA USONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA KWA UCHUNGUZI PAMOJA NA KUTAMBULIWA
NA NDUGU. JITIHADA ZA KUWATAFUTA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. JANE ANDEMBWISYE (41) MKAZI WA UYOLE KATI
NA JACKSON MLUNGU (58) MKAZI WA ITEZI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] UJAZO WA LITA 11/2.
MSAKO HUO UMEFANYIKA MNAMO TAREHE
11.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO UYOLE, KATA YA IGAWILO,
TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA
WANYWAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment