Polisi nchini Sudan wanasema kuwa
afisaa mmoja wa ubalozi wa Uhispania amepatikana akiwa amefariki baada
ya kudungwa kisu nyumbani kwake mjini Khartoum.
Afisaa huyo mwenye
umri wa miaka 60, alikuwa mkuu wa kitengo cha kutoa viza katika ubalozi
wa uhispania na alikuwa ameishi nchini Sudan kwa miaka mitatu.
Alikuwa anaishi katika mtaa wa Garden City mjini Khartoum na mwili wake ulipatikana mapema Jumatatu.
Polisi nchini Sudan pamoja na maafisa wa wizara ya mambo ya nje wamesema kuwa uchunguzi unafanywa.
Duru za kidiplomasia zinasema kuwa kifo cha afisaa huyo ni kweli kimetokea ila haijulikani nia ya mauaji yake.
Afisaa
mmoja nchini Urusi na mkewe walijeruhiwa katika tukio lengine kama hilo
lililotokea katika ubalozi wa Urusi mwezi Januari.
Hata hivyo, ni nadra kwa afisaa wa ubalozi kushambuliwa nchini Sudan.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment