Baadhi ya viungo vilivyopatikana vikiwa vimetupwa mjini Dar es Salaam

Polisi nchini Tanzania wanachunguza kisa ambapo masalia ya viungo vya binadamu yalipatikana yametupwa katika mtaa mmoja wa jiji la Dar es Salaam Jumatatu jioni.

Mwandishi wa BBC aliyezuru eneo hilo, aliambiwa na walioshuhudia masalia hayo yaliyopatikana yakiwa ndani ya mifuko ya plastiki na yakiwa yametupwa karibu na Dar es Salaam , kuwa yanaonekana kutoka kwa karibu watu 100.

Masalia hayo yalikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka mjini.

Afisa wa polisi aliyezungumza na BBC alisema kuwa masalia hayo tayari yamechulikuwa na polisi.

Polisi huyo alisema masalia hayo yalikuwa ya vidole, mifupa ya mwili na mafuvu.

Baadhi ya mifuko hiyo ilikuwa na vifaa vya kufanyia upasuaji ikiwemo glovu, na kuzua wasiwasi kuwa huenda sehemu hizo zilitoka katika taasisi ya utafiti wa kimatibabu na kutupwa kwa njia isiyofaa.

Inaarifiwa mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na kisa hicho ambacho kimewashangaza wengi mjini humo.

Tukio lenyewe liliripotiwa Jumatatu jioni.
Wakazi wanasema walianza kupatwa na wasiwasi baada ya gari lililokuwa limebeba masalia hayo kurejea katika sehemu ambapo masalia ya kwanza yalikuwa yametupwa ikiwa imebeba mifuko ya plastiki, yakiwa na karibu kilo 25.

BBC bado inasubiri kupata taarifa kutoka kwa maafisa wakuu nchini Tanzania kuhusu idadi kubwa ya masalia ya viungo vya binadamu kutupwa katika eneo la makazi ya watu kinyume na sheria.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top