Wanamgambo wa Al Shabab wamedai kuwa wamemuua kwa kumfyatulia risasi Mbunge maarufu mjini Mogadishu.
Ahmed Mohamud Hayd aliuawa baada ya kutoka
hotelini ambapo katika tukio hilo, mlinzi wake pia aliuawa na katibu wa
Bunge alijeruhiwa,mashuhuda wameeleza.
Kundi la Al-Shabab, ambalo lina
uhusiano na al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi zaidi katika
kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wanamgambo hao walipoteza ngome yao mjini
Mogadishu na kuchukuliwa na Vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2011,lakini
wameendelea kutekeleza mashambulizi ya mabomu na mauaji mjini humo.
Msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu Musab
amesema kuwa kundi lake limetekeleza mauaji kama ilivyopangwa na kuwa
wataendelea kuwafuatilia Wabunge wengine ikiwa hawataachana na Bunge.
Al-Shabab imekua ikipigania kuunda taifa la kiislamu nchini Somalia.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment