“Eeh Mungu sikia kilio changu unisaidie!” Ndivyo alivyoanza kusimulia
mtoto Salum Kassim (16), mkazi wa Kilimahewa-Tandika, Dar, ambaye
ameteseka kwa muda wa miaka minne (siku 1440) akisumbuliwa na ugonjwa wa
moyo.
Akizungumza kwa maumivu makali na wanahabari wetu nyumbani kwao
maeneo hayo, Salum alisema tatizo hilo la moyo limemsababishia matatizo
mengine ya kiafya kama moyo kujaa maji, kuvimba tumbo, kushindwa kuhema,
kukaa vizuri, kulala na kutembea.
Salum alisimulia kuwa mateso anayoyapata kupitia ugonjwa huo
yamemfanya kushindwa kuendelea na masomo kwani aliacha akiwa darasa la
tano katika Shule ya Msingi ya Moma iliyopo mkoani Mtwara, hivyo kuanza
kuhangaika na matibabu hadi mwaka 2012 alipohamishiwa Hospitali ya
Muhimbili, Dar kwa matibabu zaidi.
Alisema kuwa baada ya kufika Dar na kuanza matibabu, amejikuta
akikabiliwa na changamoto nyingi kwani kila kitu kwake ni shida kutokana
na ugumu wa maisha na kushindwa kupata matibabu ya ugonjwa wake achilia
mbali chakula na malazi.
Alieleza kuwa kuna wakati anakosa dawa kutokana na baba yake ambaye
anaishi naye kukosa fedha ya kununulia dawa na zaidi amekuwa akipata
msaada kutoka kwa mama wa jirani.
Alisema kuwa kutokana na ugonjwa huo kuna baadhi ya vyakula alivyokatazwa lakini anakula kwa sababu ya ugumu wa maisha.
Alisema kuwa kutokana na ugonjwa huo kuna baadhi ya vyakula alivyokatazwa lakini anakula kwa sababu ya ugumu wa maisha.
“Mara nyingine tunashindwa kwenda kufuata dawa kwa sababu baba mdogo anakuwa hana fedha.
“Ikitokea hivyo huwa ninakaa bila kuendelea na dozi hadi anapopata ndiyo naendelea,” alisema kwa uchungu.
“Ikitokea hivyo huwa ninakaa bila kuendelea na dozi hadi anapopata ndiyo naendelea,” alisema kwa uchungu.
Salum aliomba Watanzania wamsaidie ili apate matibabu na kurejea katika hali yake ya kawaida na kuendelea na masomo.
“Watanzania naombeni sana msaada wa hali na mali ili nipate matibabu ya huu ugonjwa kwani nimeteseka kwa kipindi kirefu.
“Ukweli sijui hatima yangu. Eeh Mungu nisaidie,” alisema.
Kaka wa Salum aliyejitambulisha kwa jina la Issa Kassim aliwaomba
wasamaria wema kumsaidia mdogo wake kwa kwa hali na mali ili kunusuru
uhai wake.
Kwa yeyote anayeguswa moyoni mwake na anaweza kumsaidia mtoto
Salum, awasiliane naye kupitia simu namba 0785999276 na 0682865248
ambazo ni za baba mdogo wa Salum aitwaye Kassim au fika katika ofisi
zetu za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar. Kutoa ni moyo si utajiri.
GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment