Maandamano na vurugu zimefanyika
leo siku ya siku ya wafanyakazi duniani katika mji mkuu wa Uturuki wa
Istanbul na maeneo mengine duniani.
Maafisa wa polisi walitumia mabomu ya kutoa
machozi pamoja na maji baada ya waandamanaji kukaidi marufuku ya
kuandamana katika bustani Taksim.
Mamia ya watu kwa makundi walikuwa
wakiandamana katika maeneo mbali mbali ya mji huo Shirika la Habari la
Associate Press limesema. Wengi wameapa kukaidi amri ya kuwazuia.
Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimewaonyesha
waaandamanaji waliobeba bendera wakiwakabili ukuta uliowekwa na polisi
wapatao 400 wa kutuliza ghasia.
Serikali ya Uturuki imewapeleka mamia ya maelfu ya maafisawa polisi pamoja na kusimamisha usafiri wa umma.
Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan mapema
aliwaonya watu walikuwa na matumaini ya kukusanyika kwenye medani ya
Taksim kuwa itaonyesha ni hatua ya kuipinga serikali.
Nako nchini Cambodia ,watu kadhaa wamedaiwa
kupigwa na polisi wanaolinda usalama walipojaribu kuvuruga maandamano ya
wapinzani waliokuwa wakiandamana katika mji mkuu wa Phnom Penh.
0 comments:
Post a Comment