Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo (kulia) akipeana mkono na Askofu Gervas John Nyaisonga.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akibusu Pete ya Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisalimiana na Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Askofu mstaafu wa jimbo la Domama Mhashamu Baba Askofu Mathias Isuja.
Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga.
Kiongozi
wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo akiwa
na Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga wakifuatilia vikundi vya
kwaya vikitoa burudani.
Waumini
na watawa wakiwa katika foeni ya kwenda kumpa mkono wa kila la kheri
aliyekuwa Askofu wa jimbo lao ambaye amehamishiwa kitume jimbo la Mpanda
Mkoani Rukwa. Kinamama wakatoliki wakiwa wamebeba zawadi ya mashine ya
kufulia nguo na Mashine ya kupoozea maji ya kunywa wakati wakielekea
kumuaga Mhashamu babab Askofu Gervas Nyaisonga.
Wanafunzi
kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Dodoma wakifuatilia sherehe za
kumuaga Askofu Gervas John Nyaisonga Katika viwanja vya kanisa la
Mkatifu Paul wa Msalaba.
Vijana wa Skauti wa Kanisa Katoliki Mkoani Dodoma wakitoa salamu kwa Askofu Gervas John Nyaisonga.
Askofu Gervas John Nyaisonga akikagua gwaride la Skauti.
Mamia ya wakotiliki wamejitokeza kumuaga
Askofu wa jimbo la katoliki Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John
Nyaisonga ambaye anahamia Mpanda kwa ajili ya kuendelea na kazi
Dini.Sherehe hiyo iliyotanguliwa na Ibada ilifanyika katika Kanisa kuu
la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mkoani Dodoma.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambayo
alikuwepo Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pina,alikuwa Kiongozi wa Kanisa
Katoliki hapa nchini,Mwadhama Polcarp Kardinal Pengo. Pia sherere hiyo
ilihudhuriwa na Askofu mstaafu wa jimbo la Domama Mhashamu Baba Askofu
Mathias Isuja.
Katika sherehe hiyo ,Mhashamu Baba Askofu
Gervas John Nyaisonga. alizawadiwa vitu mbali mbali zikiwemo fedha
taslimu. Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga anaondoka rasmi
Dodoma kuelekea Mpanda Ijumaa tarehe 2 akipitia Tabora. Amehamishiwa kwa
kazi za Kichungaji Jimbo la Mpanda.
Pamoja na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mama Rehema Nchimbi,Papadri na watawa wote wa jimbo la Dodoma
kulikuwepo vikundi vya kwaya kutoka makanisa mbalimbali ikiwemo kwaya ya
Kanisa analosali Mhe.Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Kwaya ya Shirikisho
Hananasifu Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment