Jopo la ujumbe wa Urusi kwenye Shirika la ulinzi na
Ushirikiano barani Ulaya wamesema watafanya kila njia kuhakikisha
waangalizi wa kijeshi wa Umoja wa Ulaya walioshikiliwa mashariki mwa
Ukraine wanaachiliwa huru.
Waangalizi wapatao wanane na Maafisa wengine wa
kijeshi wa Ukraine walikamatwa hapo Ijumaa na wanaharakati wanaounga
mkono Urusi katika mji wa Sloviansk.
Wapiganaji wa mji huo wanasema walioshikiliwa walikuwa wakituhumiwa kuwa walikuwa wakifanya upepelezi.
Kiongozi wa mji huo anayeunga mkono Urusi
amesema waangalizi hao wangeachiwa kwa mpango wa kubadilishana wafungwa
kwa wapiganaji waliokamatwa na majeshi ya Ukraine.
Waandishi kadhaa pia walikamatwa na kushikiliwa.
Mwandishi wa BBC aliyeshikiliwa na kuachiliwa muda mchache baadaye, amesema mji huo hauna utawala wa kisheria na kuna wasi wasi nguvu za kijeshi zikatumika.
Mwandishi wa BBC aliyeshikiliwa na kuachiliwa muda mchache baadaye, amesema mji huo hauna utawala wa kisheria na kuna wasi wasi nguvu za kijeshi zikatumika.
Marekani imesema ndege za kijeshi za Urusi zimeingia kwenye anga ya Ukraine mara kadhaa.
Bbc
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment