
Serikali ya Sudan Kusini imeelezea kwa mara ya kwanza
kuhusu idadi kubwa ya wanajeshi wake wanaoasi jeshi na kujiunga na
waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa Rais Riek Machar.
Serikali hiyo imeelezea hayo ikitaka jamii ya kimataifa kuisaidia kwa kutuma wanajeshi nchini humo ili kujaza pengo hilo.
Kinara wa serikali Tulklio Odongi
aliambia bunge siku ya Jumatatu kuwa hadi asilimia sabini ya wanajeshi
wa serikali wanageuka na kuwa watiifu kwa Riek Machar pamoja na kuasi
jeshi.
Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati na kutuma vikosi vya usalama hadi pale udhaifu huo utakapokwisha.
Bwana Odongi alimsihi Rais Salva Kiir
kuhakikisha kuna ulinzi wa kutosha wa Ardhini, angani na majini ili
kundoa wasiwasi unaosababishwa na wanajeshi wa serikali kuasi jeshi.
Kuna taarifa kuwa serikali ya Sudan Kusini inafadhili jeshi la Uganda ili kuisaidia na kupambana dhidi ya waasi.
Wakati huohuo, waasi wa Sudan Kusini wamekiri
kuwa wanajeshi wanaasi jeshi na hata kuonya kuwa wanajeshi zaidi
wanajiandaa kuhamia upande wa waasi.
Upande wa Riek Machar unasema kuwa jeshi
limekuja kujionea kuwa Rais Salva Kiir ndiye anayechochea vita huku
akisababisha mapigano yasiyo na msingi hata kidogo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment