Vimelea vya Malaria
Mwanabayologia mmoja nchini Ujerumani amesema kuwa
amepata ushahidi kuwa utawala wa Nazi uliokuwa unaongozwa na Adolf
Hitler, ulikuwa unalenga kutumia Mbu kama silaha wakati wa vita vya pili
vya dunia.
Klaus Reinhardt kutoka chuo kikuu cha übingen,
alichunguza kumbukumbu za kitengo cha utafiti kilichokuwa katika kambi
moja ya mauaji ya Dacahu mwaka 1944.
Anasema aligundua kuwa amri hiyo ilitolewa na mkuu wa kitengo cha jeshi, Heinrich Himmler.
Reinhardt anasema kuwa wanasayansi walikuwa
wanajaribu kupata Mbu ambaye angeambukizwa vimelea vya Malaria na
kuwaeneza katika maeneo ya maadui kwa wingi ili waweze kuwaambukiza watu
wengi iwezavyo.
Inajulikana kuwa wafungwa waliokuwa wanusbiri kuuawa katika kambi hiyo waliambukizwa ugonjwa wa Malaria.
Duru zinasema kuwa mipango hiyo haikufanikiwa kwa sababu wajerumani walikuwa wanashambuliwa vikali wakati huo wa vita.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment