Maelfu ya watu wameachwa bila makao kutokana na vita vya waasi visivyoisha.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, umesema kuwa zaidi ya watu sabini waliuawa
mwishoni mwa mwezi uliopita na mapema mwezi huu.
Katika mahojiano na BBC, afisa mmoja wa shirika
la Monusco, mjini Goma, Ray Tores, amesema kuwa ndege ya wanajeshi wake,
iliyokuwa ikifanya uchunguzi, katika eneo hilo iligundua kuwa vijiji
vitatu viliteketezwa na kuharibiwa kabisa.
Amesema kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa watazuru eneo hilo baadaye hii leo ili kufanya uchunguzi zaidi.
Jeshi la kutunza amani la Umoja wa Mataifa
limeimarisha juhudi zake katika eneo hilo, hasa tangu
lilipolisambaratisha kundi la waasi wa M23, Novemba mwaka uliopita.
Bwana Torres, amesema kuwa zaidi ya makundi arubaini ya waasi yanajulikana kuendesha operesheni zao katika eneo hio la Goma.
Manne kati yao yamekuwa yakifanya mashambulio ya mara kwa mara na hivyo kuwa tishio kubwa la usalama.
Umoja wa Mataifa, umesema kuwa mauaji hayo
yalitekelezwa na makundi ya waasi yaliyojihami katika mkoa wa Kivu ya
Kaskazini, ili kuwatia hofu watu wanaoishi katika eneo hilo.
Afisa huyo amesema kuwa wengi wa waliouawa walikuwa na majeraha ya mapanga.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment