
Mahakama moja mjini Cairo Misri imeahirisha kesi ya
aliyekuwa Rais Mohammed Morsi, baada ya mawakili wake kuondoka
mahakamani kwa hasira.
Mawakili hao wanalalamikia kile wanachosema ni
kuendelea kuzuiliwa kwa Morsi pamoja na waliokuwa wanachama wa vuguvugu
wa Muslim Brotherhood ndani ya chumba cha Glasi ambacho hakipitishi
sauti.
Duru zinasema kuwa mahakama itateua mawakili wengine kumtetea Morsi.
Kesi dhidi ya Morsi itasikilizwa tena Jumapili Ijayo.
Rais huyo wa zamani alipinduliwa na jeshi mwezi
Julai baada ya kutuhumiwa kwa kupanga njama na nchi za Magharibi,
utawala wa Pallestina Hamas, kundi la Hezbollah nchini Lebanon na
serikali ya Iran kupanga mashambulizi nchini Iran.
Hii ni moja ya kesi nne zinazomkabili Morsi pamoja na maafisa wakuu wa Muslim Brotherhood na iwapo atapatikana na hatia bwana Morsi anakabiliwa na hukumu ya kifo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment