
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewapa adhabu ya onyo kali makada wake sita baada kuwahoji kupitia tume yake Maadili na kuthibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa na chama kugombea Urais kabla ya wakati jambo ambalo ni kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili ya za CCM.
Pia makada hao wamepewa adhabu hiyo kwa kuthibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii. Kosa ambalo pia inaelezwa kuwa ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo.
Akizungunza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwataja waliohojiwa na Kamati hiyo kuwa ni Ndg. Frederick Sumaye (Waziri Mkuu wa zamani), Edward Lowasa, (Waziri Mkuu wa Zamani), Benard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Stephen Wassira (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais), January Makamba (Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia) na William Ngereja (Waziri wa zamani). Kupata taarifa Kamili ya CCM>BOFYA HAPA
Via Ccmblog TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment