Mamia ya manusura wa kimbunga Haiyan ambao wanahitaji msaada wa dharura

Rais wa Ufilipino Benigno Aquino ametangaza hali inayokumba nchi hiyo kama janga la kitaifa akiomba msaada zaidi kuwafikia maelfu ya walioathirika kutokana na Kimbunga Haiyan.

Katika taarifa yake, alisema kuwa maeneo mawili yaliyoathiriwa zaidi , mikoa ya Leyte na Samar, imekumbwa na uharibifu mkubwa pamoja na maelfu kupoteza maisha yao.

Maelfu ya manusura wangali wanasubiri msaada kuwafikia ambapo
takriban watu 10,000 wanahofiwa kufariki kwenye kimbunga hicho. 

Moja ya miji iliyoathirika vibaya ni Tacloban ambako mwandishi wa BBC aliye katika eneo hilo Jon Donnison, anasema kuwa hadi sasa bado hakuna mpango mzuri wa kuwawezesha watu kupata msaada.

Mamia ya amelfu ya watu wamepoteza makao yao kutokana na mawimbi makali na maji yaliyoharibu nyumba zao.

Uharibifu uliotokea katika barabara na viwanja vya ndege umetatiza zaidi juhudi za kuwafikishia misaada wale wanaoihitaji zaidi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa Umoja wa Matifa utaanzisha leo juhudi kubwa zaidi za kuwasadia waathiriwa wa kimbunga.

Aliwataka wanachama wa Umoja huo kujitolea kuwasaidia watu wa Ufilipino katika hali hii ngumu.

Kimbunga Haiyan kinaemekana kuwa kibaya zaidi kwuahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo na kilipiga siku ya Ijumaa na Jumamosi. 

Kimbunga hicho kilielekea Magharibi mwa nchi hiyo na kuzamisha visiwa sita katika eneo la Kati mwa Ufilipino. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top