Rais Barack Obama wa Marekani pamoja na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia Watanzania akiwa Dar es Salaam 
Tangu kuchukua madaraka mwezi Macdhi 2013, inaonekana utawala wa Uhuru Kenyatta umetumia kila uwezo wake wa kidiplomasia kujaribu kusitishya kesi dhidi Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa ICC.
Kutokana na hali hiyo mchambuzi wa masuala ya kisiasa Paul Mwangi anasema, kwa bahati mbaya mkakati huo wa kutumia Umoja wa Afrika kuwasilisha mapendekezo yake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unasababisha Kenya kugombana na baadhi ya marafiki na washirika wake wa muda mrefu kama Uingereza.

Akizungumza na Sauti ya Amerika juu ya makala yake ya hivi karibuni kwenye gazeti la Daily Nation, Bw Mwangi anasema Wakenya wanabidi kuamka na kutambua kwamba hali ya mambo imebadilika katika kanda yao kulingana na ilivyokua miaka 20 iliyopita.

Anasema, hadi hivi karibuni ni kweli Kenya ilikuwa mshirika mkuu wa nchi za magharibi na kila mtu alitaka kuwekeza nchini humo, lakini anasema, "hivi sasa mambo yamebadilika, kumepatikana amani Uganda, Ethopia, Sudan ya Kusini na hata Tanzania imeacha kando siasa zake za ujamaa na nchi hizo zinavutia wawekezaji kutoka nchi za magharibi na China."

Kenya kujikuta katika hali hii anasema Bw. Mwangi, ni kutokana na uongozi mbaya ambao unajaribu kuwaeleza wa Kenya kuwa mambo ni mazuri ili kuficha mizozo na kasoro zao za kisiasa na kushindwa kuleta mageuzi ya kweli. 
Chanzo: VOA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top