Wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab nchini Somali
wamesema wao ndio waliotekeleza shambulizi la bomu la kujitoa muhanga
nje ya hoteli katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia ambapo watu
sita waliuawa wakiwemo maafisa wa polisi.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amelaani
shambulio hilo lilitokea nje ya Hotel ya Maka al Mukurama huku
akisisitiza kuwa shambulio halitarudisha nyuma jihada kubwa
zinazoendelea za kuleta amani na usalama nchini humo.
Kundi hilo la Al Shabaab ambalo lilifurushwa na
majeshi ya Somalia yakishirikiana na yale ya Umoja wa Mataifa AMISOM
miaka miwili iliyopita wameapa kuendeleza harakati zao za kufanya
mashambulizi.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya ndani wa Somalia
Abdikarim Hussein Guled aliiambia BBC kuwa watu sita waliuawa na wengine
15 kujeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.
Mwandishi wa BBC Ibrahim Mohamed Adan ambaye yupo Mogadishu amesema sauti ya mlipuko ulisikika katikati ya mji huo wa Mogadishu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment