Watu wawili wamefariki na wengine takriban watu 50 kukwama kwenye vifusi baada ya paa la jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.

Inaarifiwa watu 29 wameweza kuokolewa ambapo madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.

“Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama,” alisema msemaji wa kampuni hiyo.

Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.

Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top