Hali ya wasiwasi imejitokeza kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa huduma za matibabu
katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi Kilimanjaro baada ya uongozi wa
hospitali hiyo kumkamata mtu anayejifanya kuwa ni daktari wa watoto
akiwa kwenye wodi ya upasuaji.
Daktari huyo feki aitwae Alex Sumni Massawe
amewekwa chini ya ulinzi na Jeshi la Polisi baada ya kukutana na mmoja
wa wagonjwa ambae alimuahidi kumfanyia mwanae wa kiume upasuaji wa
ngozi.
Alex anadaiwa kutaka kumfanyia upasuaji kijana MAKASI TIPESA mkazi wa Manispaa ya Moshi ambae amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa muda mrefu sasa.
Afisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC Gabriel Chisseo
amesema daktari aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo kutokana
na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambae
amekuwa akijinadi kwamba anafanya huduma hiyo hospitalini hapo.
Chisseo
anasema ‘Katika jitihada za wazazi kumuokoa mtoto wao wakawa
wamewasiliana na mtu mmoja mtaani aliwapa namba ya huyu daktari feki
kwamba angewasaidia, walipokutana nae alisema wamlipe shilingi laki tatu
ili afanye huo upasuaji hospitalini KCMC ambapo alitanguliziwa laki
mbili za kuanzia’
Uongozi
wa Hospitali ya KCMC umethibitisha kwamba mtu huyo aliyekamatwa ndani
ya Hospitali hiyo si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala
kitambulisho kinachomtambulisha kitengo chake cha kazi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amethibitisha jeshi hilo kumtia mbaroni Alex.
Via Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment