Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama Joseph Ole Lenku imesema kuwa watu 59 wamefariki katika shambulizi la kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.

Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano na haijulikani ikiwa wanawazulia waathiriwa au waathiriwa wamjificha katika sehemu mbali mbali za jumba la Westgate.

Shirika la Red Cross awali katika taarifa yake ilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika mashambulizi la kigaidi Jumamosi mchana.

Milio ya risasi imeweza kusikika katika jengo la Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawazuilia mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa.

Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika ufyatulianaji huo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku watu wawili wakinusuriwa asubuhi ya leo.

Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaribu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya jengo hilo.

Watu 39 wameuawa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo hilo mwanzo katika eneo la kuegeshea magari na kisha kuingia ndani ya mikahawa na maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwapiga watu risasi kiholela.

Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.

Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa. Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.

Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa walifariki kutokana na majeraha yao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top