Wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria
Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram
wamewauwa takriban watu ishirini wanachama wa makundi kadhaa ya ulinzi
waliokuwa wakipinga kundi hilo Kaskazini mwa jimbo la Borno.
Wakuu wa jeshi la nchi hiyo wanasema vifo hivyo vilitokea katika mashambulio mawili tofauti siku ya Jumapili na Jumatatu ambapo kundi hilo la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulio nchini Nigeria tangu mwaka wa 2009.
Mwezi Mei mwaka huu, rais wa nchi hiyo Goodluck
Jonathan, alitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ta Kaskazini
Mashariki mwa nchi hiyo, akisema kundi hilo la Boko Haram linahatarisha
usalama wa taifa hilo.
Jeshi la nchi hiyo lilianzisha operesheni kali
ya kuwasaka wapiganaji wa kundi hilo, ambalo linataka kuundwa kwa taifa
huru litakalozingatia sheria za Kiislamu maarufu kwama Sharia.
Jeshi la nchi hiyo lilihimiza wakaazi wa majimbo hayo kuunnda makundi ya raia ili kukabiliana na kundi hilo endapo watawavamia.
Lakini kwa sasa kundi hilo la Boko Haram,
linaonekana linalipiza kisasi dhidi ya makundi hayo ya kiraia na hivyo
kuongeza wasi wasi kuwa kuundwa kwa makundi hayo huenda kukachochea
ghasia zaidi nchini humo.
Siku ya Jumapili, watu waliokuwa na sare rasmi
za jeshi la nchi hiyo walivamia mkutano wa kundi moja la ulinzi wa
kiraia na kuwafyatulia risasi na kuwauawa watu kumi na wanne.
Afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo ameliambia
shirika la habari la AFP kuwa watu wengine wanne waliuawa kwenye
shambulio lingine siku ya Jumatatu usiku katika kijiji cha Borno,
wilayani Damasak.
Wapiganaji hao waliwashambulia wanachama wa
kundi lingine linalojiita jeshi la wanainchi au Civilian Joint Task
Force wakiwa usingizini katika hoteli moja.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment